China yataka Marekani irekebishe makosa na kuonyesha udhati kwa ajili ya mazungumzo ya kijeshi
2023-05-31 08:41:20| CRI

China imeitaka Marekani irekebishe haraka makosa yake kwa vitendo, na kuonyesha udhati kwa ajili ya mazungumzo kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning alipozungumzia hoja iliyotolewa na Marekani kwamba China imekataa ombi la Marekani la kufanyika kwa mazungumzo kati ya mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili pembezoni mwa mazungumzo ya Shangri-La chini Singapore.

Mao Ning amesema Marekani inafahamu vya kutosha ni kwa nini mazungumzo ya kijeshi kati ya China na Marekani yanakabiliwa na changamoto, ni lazima Marekani iheshimu mamlaka, usalama na ufuatiliaji wa China na kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya mazungumzo hayo.