Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya jana imelaani vikali kitendo cha Ubalozi wake nchini Sudan kuvamiwa na baadhi ya vifaa kuibiwa.
Katika taarifa yake, Wizara hiyo imesema uvamizi na uporaji katika jengo la Ubalozi wake mjini Khartoum ni ukiukaji wa Mkataba wa Vienna wa Uhusiano wa Kidiplomasia, na sheria na kanuni zote zinazosimamia kazi za kidiplomasia kati ya nchi.
Taarifa hiyo imetoa wito kwa pande zinazopigana nchini Sudan kuacha vurugu na mapigano, kulinda tume za kidiplomasia, na kutatua tofauti zao kwa njia ya majadiliano na amani.