Rais Xi Jinping ahimiza juhudi za kufanya uwezo na mfumo wa usalama wa taifa wa China kuwa wa kisasa
2023-05-31 08:39:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuharakishwa kwa juhudi za kufanya uwezo na mfumo wa usalama wa taifa kuwa wa kisasa.

Rais Xi ameyasema hayo wakati akiongoza mkutano wa kwanza wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa iliyo chini ya Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambayo yeye ni mwenyekiti wake.

Rais Xi ametoa wito wa kuendelea kufahamu kwa kina hali ngumu na changamoto zinazokabili usalama wa taifa na kufahamu kwa usahihi masuala muhimu ya usalama wa taifa.

Amehimiza juhudi za kulinda muundo mpya wa maendeleo wa China, kwa utaratibu mpya wa usalama na kuwa na mafanikio mapya kwenye kazi za usalama wa taifa.