Wachimbaji wanne wa madini wamekufa kwa kufunikiwa na kifusi walipokuwa wakiendelea na shughuli ya kuchimba dhahabu katika eneo la Mwasabuka, Wilaya ya Nyang’hwale, mkoani Geita nchini Tanzania.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyang’hwale, Fabian Sospeter amesema, watu watatu walifariki dunia papo hapo wakati mwingine alipoteza maisha wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka mamlaka za madini na Jeshi la Polisi, vifo vya wachimbaji hawa vinafikisha idadi ya vifo 13 vya wachimbaji wadogo vilivyoripotiwa mkoani Geita katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka huu.