Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa larefusha muda wa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini
2023-05-31 08:38:56| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kurefusha kwa mwaka mmoja vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan Kusini, ikiwa ni pamoja na vikwazo vinavyolenga vya marufuku ya kusafiri na kufungia mali za watu binafsi na mashirika hadi Mei 31 mwaka 2024.

Azimio nambari 2683 lililopitishwa kwa kura 10 za ndio na tano za kutopigwa pia linaamua kurefusha muda wa Jopo la Wataalamu, linalosaidia kazi ya Kamati ya Vikwazo ya Sudan Kusini hadi Julai 1, mwaka 2024. China, Gabon, Ghana, Msumbiji na Russia hazikupiga kura.

Azimio linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya mashauriano karibu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na Jopo la Wataalamu, kabla ya Aprili 15 mwaka 2024, kutathmini maendeleo yaliyofikiwa kwenye vigezo muhimu vilivyowekwa katika Azimio 2577 lililopitishwa mwaka 2021.

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang amesema kuwa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini vimekuwa na utata mwingi.