WHO yaipongeza Tanzania kwa kupambana na magonjwa ya milipuko
2023-05-31 20:26:39| cri

Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tedros Ghebreyesus ameipongeza Tanzania kwa juhudi inazoendelea kufanya katika kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kuingia na kuenea nchini humo.

Dk. Tedros amesema hayo kwenye kikao maalum na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Marzui pamoja na wataalamu wengine katika sekta ya afya. Dk Tedros ameipongeza Tanzania kwa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Marburg na kwa kushirikiana na WHO katika kuimarisha huduma za uchunguzi na udhibiti dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Tanzania imeungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa chini ya WHO kushiriki kikao cha 76 cha Shirika la Afya Duniani kinachofanyika mjini Geneva, Uswisi.