Mara nyingi wanawake hawajishughulishi na mazoezi, lakini katika zama hizi, wimbi la wanawake wanaofanya mazoezi na kufuatilia lishe bora limeendelea kuongezeka. Baadhi ya wanawake wanabadili mtindo wao wa maisha kutokana na magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, na mengine, huku wengine wakiamua kubadili mtindo wa maisha kutokana na hofu ya kupata magonjwa.
Kwa hapa China, mara nyingi, hususan wakati wa majira ya mchipuko na majira ya joto, utaona vikundi vya wanawake wakicheza katika bustani ama maeneo ya wazi. Dansi hii wengi wanaichukulia kama sehemu ya mazoezi, na kuipa nafasi muhimu katika ratiba zao za siku. Kutokana na hayo, kipindi chetu cha leo cha Ukumbi wa Wanawake kitazungumzia zaidi umuhimu wa mazoezi na lishe bora kwa wanawake.