Rais Xi atembelea shule ya Beijing kabla ya siku ya Watoto ya Kimataifa
2023-06-01 08:37:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametembelea shule moja mjini Beijing kabla ya Siku ya Watoto ya Kimataifa, ambayo inaadhimishwa Juni 1.

Rais Xi amesisitiza maendeleo ya pande zote ya watoto katika zama mpya, na kutoa salamu za siku ya watoto nchini kote.

Katika ziara yake katika Shule ya Yuying ya Beijing, rais Xi amesema watoto ni mustakabali wa nchi na tumaini la taifa. Amesisitiza kuwa msingi mzuri wa maadili ya watoto, uwezo wa kiakili, nguvu ya mwili, usikivu mzuri na ustadi wa kazi ni muhimu.

Rais Xi amewataka watoto wa China katika zama mpya kuwa na matarajio na ndoto za juu, kufurahia kusoma na kufanya kazi, kuwa na shukrani na urafiki, na ujasiri wa kuvumbua na kufanya juhudi.

Aidha ameeleza matumaini yake kuwa wanafunzi hao watasoma kwa lengo la kujenga nchi imara na kuchangia katika ufufuaji wa taifa, na kukidhi matarajio ya wazazi wao, Chama na wananchi.