Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Mao Ning amesema China inaunga mkono juhudi za serikali ya Mali za kupambana na ugaidi na kulinda usalama na utulivu wake.
Habari zinasema taasisi husika hivi karibuni iliripoti kuhusu matukio katika kijiji cha Moura ikionyesha kwamba vikosi vya Mali na mamluki wa kigeni walikiuka haki za binadamu katika operesheni dhidi ya ugaidi.
Akizungumzia hili, Bi. Mao amesema China daima inatetea kwamba pande zote zinapaswa kufanya mazungumzo ya kiujenzi na ushirikiano kuhusu masuala ya haki za binadamu, na kupinga kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha haki za binadamu.