Karakana ya Luban nchini Ethiopia: Mfano mzuri wa Elimu ya Ufundi Stadi ya China kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
2023-06-01 09:29:22| CRI

Habari za wakati huu msikilizaji na karibu kwenye kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Kipindi cha leo msikilizaji, licha ya habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti inayohusu karakana ya Luban nchini Ethiopia, ambayo inachukuliwa kama mfano mzuri wa Elimu ya Ufundi Stadi ya China kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yatakayohusu warsha ya kila mwaka ya kuwapa ajira wanafunzi wanaohitimu masomo yao katika taaluma mbalimbali na kushirikisha kampuni nyingi za kigeni, ikiwemo kampuni ya Huawei ya China.