Mkurugenzi anayeshughulikia kudhibiti migogoro wa Idara ya Masuala ya Kisiasa Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika Bw. Alhadji Sarjoh Bah, amesema Sudan na watu wake wanatakiwa kushughulikia malalamiko ya kimfumo ambayo yamekuwepo kwa miongo kadhaa iliyopita.
Akiongea kwenye mkutano wa tatu wa utaratibu uliopanuliwa wa kushughulikia mgogoro wa Sudan, Bw. Bah amesema kuna haja ya kuanza kupanga na kujiandaa kwa mazungumzo jumuishi kuhusu mchakato wa kisiasa, utakaoshughulikia sababu za sasa na za muda mrefu za mgogoro wa Sudan.
Pia amesema licha migongano kuhusu mageuzi ya sekta ya usalama ndio yamechochea mgogoro huo, Sudan na Wasudan wanahitaji kushughulikia malalamiko ya kimfumo ambayo yalianza miongo kadhaa iliyopita.