Wataalamu wakutana nchini Zambia kujadili hatua za kuendeleza sekta ya kilimo barani Afrika
2023-06-02 23:08:43| cri

Mkutano wa ngazi ya juu wa Sera za Uongozi za Kilimo barani Afrika umefanyika jana alhamis katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, kwa lengo la kujadili changamoto zinazoathiri maendeleo ya kilimo katika bara la Afrika, na kutafuta suluhisho la kuendeleza zaidi sekta hiyo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema, licha ya kilimo kuwa chanzo kikuu cha maisha na kipato barani Afrika, utendaji wake umeendelea kuathiriwa na changamoto mbalimbali. Amesema sekta ya kilimo barani Afrika inakabiliwa na changamoto kama kiwango duni cha mashine na umwagiliaji, uhaba wa fedha kwa ajili ya shughuli za kilimo, uwekezaji mdogo katika masuala ya utafiti na maendeleo ya kilimo.

Amezitaka nchi za Afrika kutunga sera bora na kuongeza uwekezaji utakaochochea ukuaji na ushirikiano jumuishi katika mnyororo wa thamani wa bidhaa za kilimo.