Peng Liyuan na wake wa marais wa Afrika wazindua kampeni ya afya kwa watoto yatima barani Afrika
2023-06-02 09:02:42| CRI

Mke wa Rais Xi Jinping wa China Bi. Peng Liyuan, na Shirika la Marais Wanawake wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD) kwa pamoja wameanzisha kampeni ya huduma ya afya kwa watoto yatima wa Afrika "Kufurahisha Mioyo ya Watoto: Hatua ya Pamoja ya China na Afrika" kabla ya Siku ya Watoto ya Kimataifa.

Mabalozi wa China na timu za matibabu katika nchi za Afrika wametembelea watoto katika vituo vya watoto yatima na taasisi zinazohusika, kufanya shughuli kama vile uchunguzi wa matibabu bila malipo na kutoa msaada wa mifuko ya huduma.

Akielezea kuhusu shughuli za hisani Bi. Peng alisema, China ni rafiki na mshirika wa dhati wa Afrika. Mwaka huu inatimia miaka 60 tangu kuanza kutumwa kwa timu za matibabu barani Afrika na serikali ya China. Timu za matibabu za China zimesaidia kikamilifu watu wa nchi za Afrika na kuwa wajumbe wa kuendeleza urafiki kati ya China na Afrika.

Rais wa zamu wa OAFLAD ambaye pia ni mke wa rais wa Namibia Bi. Monica Geingos na wanachama wa shirika hilo waliitikia vyema na kutoa shukrani kubwa kwa huduma za muda mrefu na uungaji mkono wa Bi. Peng kwa maendeleo ya wanawake na watoto katika Afrika.