Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa BRICS wafunguliwa Afrika Kusini
2023-06-02 09:15:16| CRI

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa BRICS umefanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Alipoendesha mkutano huo, waziri wa uhusiano na ushirikiano wa kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor amesema, wataangazia fursa za kuimarisha na kubadilisha mifumo ya utawala wa kimataifa, na kutazamia suluhisho la ufufuaji wa uchumi wa dunia endelevu na shirikishi.

Ameongeza kuwa mkutano wa wakuu wa nchi za BRICS wa mwaka huu utafanyika Johannesburg, chini ya kaulimbiu ya "BRICS na Afrika: wenzi wa kutafuta ukuaji wa kasi wa pamoja, maendeleo endelevu na ushirikiano shirikishi wa kimataifa."