Mapigano kati ya kikosi cha waasi cha Sudan na kikosi cha RSF zimeendelea katika mji mkuu Kartoum na sehemu za jirani, mapigano katika kusini mwa Khartoum, mashariki mwa Khartoum na sehemu ya kaskazini mwa mji wa Khartoum yamekuwa makali zaidi.
Katika eneo la Darfur, mapigano kati ya pande mbili yameendelea kwa siku kumi kadhaa. Kiongozi wa eneo hilo tarehe 4 ametangaza kuwa, majimbo 5 ya eneo hilo yameingia kwenye hali ya maafa, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa dharura wa kibinadamu.