China yatafuta njia ya maendeleo ya amani lakini kamwe haitaacha kulinda haki na maslahi yake halali
2023-06-05 08:54:04| CRI

Mazungumzo ya 20 ya Shangri-La yamefanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 Juni nchini Singapore. 

Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu alipotoa hotuba kuhusu “Mapendekezo mapya ya usalama ya China” amesisitiza kuwa, China inatafuta njia ya maendeleo ya amani, lakini kamwe haitaacha kulinda haki na maslahi yake halali, hasusan maslahi makuu ya nchi. Pia amenukuu wimbo mmoja unaojulikana sana nchini China usemao: “Marafiki wanapokuja wanakaribishwa kwa divai tamu, wanyama wakali wakija watapigwa risasi.”