Wataalamu kutoka ujumbe wa China kwenye Mazungumzo ya Shangri-La: China iko hapa kwa ajili ya maendeleo ya amani na ushirikiano
2023-06-05 18:59:13| cri

Mazungumzo ya 20 ya Shangri-La yalifungwa Juni 4 nchini Singapore. Walipokutana na wanahabari baada ya mazungumzo hayo, wataalamu wa ujumbe wa China wamesema kuwa China imetoa mchango chanya katika kudumisha amani ya dunia na kutoa bidhaa zaidi za usalama wa umma kwa jumuiya ya kimataifa. Wajumbe wa China wameshiriki kwenye mkutano huo kwa ajili ya kuendeleza amani na ushirikiano.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Taifa ya China Bw. Tan Kefei amesema, katika mkutano huo China ilibadilishana maoni na viongozi wa idara za ulinzi au wakuu wa ujumbe kutoka Mongolia, New Zealand, Ufilipino, Kambodia, Malaysia, Ujerumani, Uingereza, Australia, Japan, Korea Kusini, Indonesia, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine kuhusu uhusiano wa pande mbili, hali ya kimataifa na kikanda, na masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja kama vile suala la Taiwan na Bahari ya Kusini ya China. Wataalamu wa China pia walifafanua dhana ya "Mpango Mpya wa Usalama wa China" kwa vyombo vya habari.

Mtaalamu wa kijeshi wa China Bw. He Lei amesema pendekezo la usalama wa kimataifa ni nyenzo halisi inayoakisi dhana ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja kwenye nyanja ya usalama wa kimataifa, ambayo inaeneza mtazamo wa usalama wa pamoja, wa jumla, wa ushirikiano na ulio endelevu.

Wataalamu wa China wamesema kuwa Mazungumzo ya Shangri-La ni jukwaa la kujadili usalama, sio maonyesho ya kuchochea umwamba. Ujumbe wa China umehudhuria mazungumzo hayo kwa ajili ya amani, maendeleo na ushirikiano.