Ethiopia yazindua mashindano ya "Daraja la Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari
2023-06-05 08:53:33| CRI

Mashindano ya lugha ya Kichina yajulikanayo kama "Daraja la Kichina" kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu vya Ethiopia yalifanyika Jumamosi.

Mashindano hayo yameandaliwa na Ubalozi wa China nchini Ethiopia, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa (AAU) na Taasisi ya Confucius katika Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET). Katika hafla hiyo, washiriki walitakiwa kutoa hotuba na kuonesha ujuzi wao.

Jumla ya wanafunzi 16 kutoka vyuo vikuu vitatu vya Ethiopia na wanafunzi sita wa shule za sekondari walihudhuria hafla ya kila mwaka ya kuzungumza na maonesho ya Kichina duniani kote.

Balozi wa China nchini Ethiopia Zhao Zhiyuan alisema washindani hao watakuwa "mabalozi" wa kuimarisha uhusiano kati ya watu na watu kati ya nchi hizo mbili.

Akihutubia shindano hilo, Terefe Belay, Mkurugenzi wa Udhamini wa masomo na Uhusiano wa Kimataifa katika Wizara ya Elimu ya Ethiopia, alisema ushirikiano wa China unazidi kutoa msukumo chanya katika sekta ya elimu ya Ethiopia, huku kukiwa na fursa za ufadhili zinazoongezeka kwa wanafunzi wa Ethiopia.