Polisi wa Nigeria jana walisema kwamba vijiji kadhaa katika Jimbo la Sokoto, kaskazini-magharibi mwa Nigeria vilishambuliwa na wanamgambo na kuua wanakijiji 30.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi wa Jimbo la Sokoto jana, watu wote waliouawa walikuwa ni wanachama wa kikundi cha wanamgambo katika wilaya ya Tangaza jimboni humo. Juni 3 kikundi hicho kiliwatuma wanachama wake kwenda kwenye jamii ambayo wengi wao ni wafugaji katika Wilaya hiyo, ili kufanya shughuli za kutoa tahadhari ya usalama, wakati shughuli hizo zinaendelea wafugaji walipigwa na kusababisha kutoridhika. Baada ya wanamgambo kurudi nyumbani, kijiji chao kilivamiwa na watu wenye silaha wanaosadikiwa kuwa wamekusanywa na wafugaji.