China kamwe haitakubali hali ya kanda ya Asia na Pasifiki ivurugwe
2023-06-05 08:51:16| CRI

Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu amesema baadhi ya nchi zilijaribu kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine na ya kanda nyingine, kuweka vikwazo kwa upande mmoja na kuzusha mapinduzi na vita, na kuondoka bila ya kuwajibika baada ya kuvuruga hali ya kanda hiyo.

Waziri Li ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mazungumzo ya 20 ya Shangri-La yaliyofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 Juni nchini Singapore, na kusisitiza kuwa China kamwe haitakubali mambo kama hayo yatokee katika kanda ya Asia na Pasifiki.