Maonyesho ya 31 ya kimataifa ya TEHAMA ya China yafanyika Beijing
2023-06-05 22:58:02| cri

Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya China yalifunguliwa Juni 4 katika Kituo cha Mikutano cha Taifa mjini Beijing. Maonyesho hayo yenye kauli mbiu ya “Kuunganisha njia kuu ya mawasiliano, kujenga kwa pamoja zama mpya ya digitali ya kisasa” yameshirikisha mashirika takriban 400 ya ndani na nje, ambako yanaonyesha matokeo mapya ya uvumbuzi ya miundombinu, teknolojia, matumizi, vifaa, na usimamizi wa kidigitali kwenye sekta za utengenezaji bidhaa viwandani, afya, elimu, nishati, uchukuzi, kilimo, fedha, utamaduni na utalii na nyinginezo.