China yaadhimisha miaka 4 tangu teknolojia ya 5G ianze kutumika kibiashara
2023-06-06 22:47:45| cri

Leo tarehe 6 Julai ni maadhimisho ya miaka 4 tangu Wizara ya Viwanda na TEHAMA ya China kutoa leseni ya matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G.

Mpaka sasa, China imejenga mtandao mkubwa zaidi na wenye teknolojia wa kisasa zaidi wa 5G kote duniani. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili, vituo milioni 2.73 vya 5G vimejengwa, na teknolojia ya 5G imetumika katika sekta 60 nchini China.