Wanadiplomasia wa China na Marekani wakutana Beijing
2023-06-06 14:47:14| cri

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Ma Zhaoxu, na mkurugenzi wa idara ya Marekani na Atlantiki ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Yang Tao wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia mambo ya Asia na Pasifiki Daniel J. Kritenbrink na msaidizi maalum wa rais wa Marekani kuhusu mambo ya China na Taiwan Sarah Beran ambao wameanza ziara nchini China Juni 5.

Pande hizo mbili zimefanya mawasiliano ya wazi, kiujenzi na yenye ufanisi kuhusu kuhimiza na kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kutatua tofauti kati yao kwa kufuata makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili mwezi Novemba mwaka jana katika kisiwa cha Bali. China imeeleza msimamo wake kuhusu suala la Taiwan na masuala mengine muhimu. Pande mbili zimekubaliana kudumisha mawasiliano.