Rais Xi Jinping afanya ukaguzi katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani
2023-06-06 21:25:47| CRI

Rais Xi Jinping wa China Jumatatu amefanya ukaguzi katika Ziwa Wuliangsu, Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, ili kufahamu zaidi matokeo ya hatua mbalimbali zilizotekelezwa katika kurejesha mazingira ya ikolojia ya huko. Hivi sasa eneo hilo lina aina 264 za ndege na aina 22 za samaki.

Rais Xi pia alikagua eneo la kielelezo la mambo ya kisasa ya kilimo lililoko kwenye ukingo wa kusini wa Ziwa Wuliangsu. Hivi sasa eneo hilo linasimamia na kupanda mazao ya kilimo kwa kutumia akili bandia.

Aidha Rais Xi alitembelea misitu ya Xinhua iliyoko huko Bayannao’er. Hadi sasa jumla ya hekta 2,600 za miti imepandwa, na kufikia asilimia 65 ya eneo la jumla.