Rais wa Honduras kufanya ziara nchini China
2023-06-06 20:49:03| cri

Habari kutoka Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imesema, rais Xiomara Castro wa Honduras jana jumatatu kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter, amesema kuwa atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 9 hadi 14 mwezi huu. Shirika la habari la Reuters limesema, hii itakuwa ziara ya kwanza ya rais wa Honduras nchini China tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.