Baraza la Usalama la UM laitisha mkutano wa dharura kufuatia shambulizi dhidi ya bwawa la Kakhovka
2023-06-07 22:29:57| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limeitisha mkutano wa dharura kufuatia shambulio dhidi ya Bwawa la Kakhovka lililosababisha bwawa hilo kubomoka.

 

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Martin Griffiths amesema, kushambuliwa kwa bwawa la Kakhovka ni tukio baya zaidi la mashambulizi dhidi ya miundombinu ya umma tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Ukraine na Russia, na kutaathiri vibaya kando mbili za mto Dnieper katika siku kadhaa zijazo. Amesema kuwa Umoja wa Mataifa utatoa msaada kwa raia zaidi lefu 16 wanaoathiriwa na shambulizi hilo.

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema, China inafuatilia kwa karibu taarifa za kuharibiwa kwa bwawa la Kakhovka na kueleza wasiwasi wake kuhusu athari za kibinadamu, kiuchumi na kimazingira. Amesema China inazitaka pande zote zinazopambana kufuata sheria ya kibinadamu ya kimataifa, kujitahidi kulinda usalama wa raia na miundombinu ya umma.