Maonyesho ya kimataifa ya droni yafanyika mjini Shenzhen, China
2023-06-07 18:30:33| cri

Maonyesho ya 8 ya kimataifa ya droni ya Shenzhen yamefanyika tarehe 4 Juni mwaka 2023.

Kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 4 Juni, maonyesho ya 7 ya droni duniani na maonyesho ya 8 ya droni ya kimataifa ya Shenzhen, yamefanyika katika kituo cha mikutano na maonyesho cha Shenzhen, mkoani Guangdong, China. Kampuni zaidi ya 300 za ndani na nje ya China zimeonyesha vifaa vipya vya droni katika maonyesho hayo.