Maafisa wa serikali, viongozi wa kisekta na watafiti walikutana Jumanne pembeni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Makazi unaoendelea jijini Nairobi, Kenya, ili kutafuta uungaji mkono wa kuhimiza uchakataji wa taka na kutumia tena pamoja na kutoa nafasi za ajira katika kukuza uchumi wa mzunguko.
Washiriki hao walijadiliana kuhusu ushirikiano katika kukuza usimamizi bora wa taka kwa nchi za Afrika ili kuhifadhi mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu wa Kenya, Festus Ng'eno, alisema sera thabiti pamoja na ufadhili, matumizi ya teknolojia na ubunifu, ni mambo muhimu katika kukuza uchumi wa mzunguko wa Afrika.
Naye afisa mtendaji mkuu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, John Bosco Kalisa, alisema kuwa usimamizi endelevu wa taka ni muhimu katika kufikia mustakabali wa kijani, ustahimilivu, ustawi na shirikishi kwa miji ya Afrika.