Nchi tano zachaguliwa kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la UM
2023-06-07 18:32:47| cri

Nchi wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana jumanne zilipiga kura na kuchagua wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2024 hadi 2025.

Sierra Leone, Algeria, Korea Kusini, Slovenia, na Guyana zilipata theluthi mbili ya kura, na kuwa wanachama wapya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Nchi hizo tano zitachukua nafasi za sasa za Albania, Brazil, Gabon, Ghana na Umoja wa Falme za Kiarabu kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2024.