Benki ya Dunia yapandisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka 2023 hadi asilimia 5.6
2023-06-07 19:32:07| cri

Benki ya Dunia jana jumanne ilitoa ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia ikipandisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka 2023 hadi asilimia 5.6.

Ongezeko hilo ni zaidi ya makadirio ya awali ya asilimia 4.3 yaliyotolewa katika ripoti hiyo ya mwezi Januari mwaka huu, na asilimia 5.1 ya “Ripoti ya nusu mwaka kuhusu uchumi wa maeneo ya Asia Mashariki na Pasifiki” iliyotolewa mwezi Aprili mwaka huu.

Aidha, ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia imeongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Marekani kwa mwaka huu hadi kufikia asilimia 1.1, na kwa nchi zinazotumia Euro makadirio hayo yameongezwa hadi kuwa asilimia 0.4.