Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika kutoa ripoti ya biashara kwa mara ya kwanza
2023-06-07 08:58:50| cri

Maonyesho ya 3 ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yatafanyika mjini Changsha kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 2 Julai. Katika kipindi hicho, ripoti ya biashara kati ya China na Afrika itatolewa kwa mara ya kwanza ili kusaidia makampuni yanayotaka kufanya biashara na Afrika.

Kaulimbiu ya maonyesho haya ni "kutafuta maendeleo ya pamoja na kunufaika na mustakabali wa pamoja", ambapo nchi 8 za Afrika zikiwemo Benin, DRC, Madagascar, Malawi, Morocco, Msumbiji, Nigeria na Zambia, zimealikwa.