Zimbabwe yapenda kuimarisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali
2023-06-08 08:57:25| CRI

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema nchi yake inapenda kuimarisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali, ili kukuza urafiki wa jadi kati ya pande mbili.

Rais Mnangagwa amesema hayo alipokabidhiwa kitambulisho cha taifa kilichowasilishwa na balozi mpya wa China nchini humo Zhou Ding. Pia amesisitiza kuwa Zimbabwe itafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na kushirikiana na China kuendeleza ushirikiano katika sekta mbalimbali chini ya mfumo wa mapendekezo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja na Maendeleo ya Dunia.

Kwa upande wake Zhou Ding amesema China itaendelea kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya pande hizo mbili kupata maendeleo mapya, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.