China yapinga serikali ya Japan kumwaga maji taka ya kituo cha kuzalisha umeme kwa nyuklia cha Fukushima baharini
2023-06-08 08:54:55| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema, ingawa serikali ya Japan ilishikilia kusema maji taka yaliyotoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima hayana sumu, na kumwaga maji hayo baharini ni chaguo pekee, lakini habari zilizotolewa na vyombo vya habari vya Japan, zinaeleza kuwa samaki wa baharini waliovuliwa kwenye bandari ya kituo hicho wamevuka viwango vya vitu vya mionzi.

Bw. Wang amesisitiza kuwa hatua hiyo ya ubinafsi ya Japan imeharibu maslahi ya pamoja ya binadamu, kuathiri vibaya raia wa nchi jirani na nchi za visiwa za bahari ya Pasifiki, na kupunguza uaminifu wa Japan duniani.