Jeshi la Chad lilisema jana kuwa vikosi vyake vimewaua waasi 23 katika mapigano makali yaliyoendelea kwa wiki moja katika mkoa wa Tibesti uliopo kaskazini.
Msemaji wa jeshi Bw. Azem Bermandoa Agouna alisema kuwa askari wanane wa serikali walijeruhiwa, na magari sita ya waasi yalikamatwa wakati wa mapigano na kundi la FNDJT na kundi la CCMSR ambayo yalianza tarehe 31 Mei.