Xi atuma barua kwenye kongamano la “Kujenga Nguvu ya Utamaduni wa China” akisitiza maendeleo ya kiutamaduni
2023-06-08 08:56:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwenye Kongamano la kwanza la “Kujenga Nguvu ya Utamaduni wa China”, lililofunguliwa jana Jumatano huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China.

Katika barua yake, Xi, alitoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kubeba jukumu jipya la kiutamaduni, na kutoa nguvu kubwa ya kiutamaduni na kiakili ili kujenga taifa lenye nguvu na kuweza kulistawisha taifa. Aidha alitaka kuunganishwa kwa imani ya kiutamaduni, kuendela kuwa wazi na jumuishi, kuzingatia kanuni za kimsingi na kuweka msingi mpya, na kuhimiza uvumbuzi wa kitamaduni na ubunifu wa taifa zima.

Alisema ni muhimu kuendelea kuimarisha ustawi wa kiutamaduni, kuifanya China kuwa nchi inayoongoza katika utamaduni, kujenga ustaarabu wa kisasa wa China na kuendeleza mawasiliano na kujifunza kati ya ustaarabu.