Jumba la kwanza la makavazi la kidigitali la kitaifa kwenye vyuo vikuu vya China laanza kutumika mjini Chongqing
2023-06-09 23:31:05| cri

Jumba la makavazi la kidigitali la kitaifa lililoko katika Chuo Kikuu cha Kusini Magharibi kilichoko mjini Chongqing, limeanza kutumika rasmi tarehe 8 Juni 2023, ambalo ni la kwanza la aina yake lililoko katika vyuo vikuu vya China.

Jumba hilo linasimamiwa kwa kutumia teknolojia za kisasa za Tehama, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya Internet of Things (IoT) na akili bandia, na mifumo ya kisasa ya usalama pia inatumika ili kuhakikisha usalama wa nyaraka na data zinazohifadhiwa katika makavazi hayo.