Uganda yapongeza uamuzi wa Kenya wa kurefusha reli hadi mji wa mpakani
2023-06-09 08:56:13| CRI

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amepongeza uamuzi wa mwenzake wa Kenya William Ruto wa kurefusha reli ya SGR kutoka Naivasha hadi mji wa mpakani wa Malaba.

Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Rais Museveni amesema serikali ya Uganda itaharakisha ujenzi wa reli hiyo kutoka Malaba hadi Kampala kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2023/24.

Wakati reli ya SGR itakapokamilika nchini Uganda, itaunganisha Uganda na nchi jirani za Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.