Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kuchukuliwa hatua kali zaidi za kulinda bahari
2023-06-09 08:54:00| cri

Tarehe 8 Juni ni Siku ya Bahari Duniani. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alitoa hotuba kwa njia ya video siku hiyo hiyo, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kali zaidi kulinda bahari.

Bw. Guterres alisema, rasilimali za baharini hudumisha ustawi wa jamii na afya ya binadamu duniani kote. Binadamu wanapaswa kuwa rafiki bora wa bahari. Lakini sasa, wamekuwa adui yake mbaya zaidi.

Bw. Guterres pia alisema, makubaliano ya kisheria ya kimataifa ya kukomesha uchafuzi wa plastiki yanajadiliwa. Mwezi Machi mwaka huu, nchi mbalimbali zilifikia "Mkataba wa Bahari Kuu  " juu ya uhifadhi na matumizi endelevu ya viumbe hai vya baharini katika maeneo yaliyo nje ya mamlaka ya kitaifa.