Mashirika mawili ya kimataifa yaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka 2023
2023-06-09 21:30:01| cri

Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), lenye makao yake makuu mjini Paris, nchini Ufaransa, hivi karibuni limetoa ripoti ya mtazamo wa uchumi wa dunia, na kupandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China hadi 5.4% mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.1 ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa mwezi Machi.

Benki ya Dunia pia ilitoa Ripoti ya Matarajio ya Kiuchumi Duniani na kupandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China hadi 5.6% mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 1.3 kutoka makadirio ya mwezi Januari. Ripoti hiyo imesema, ukuaji wa uchumi katika nchi za Asia Mashariki na Pasifiki unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 3.5 mwaka 2022 hadi asilimia 5.5 mwaka 2023. Ukuaji wa uchumi wa China umeongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka huu, mauzo ya rejareja yamepanda kwa kasi na ukuaji wa uzalishaji viwandani umeongezeka kwa wastani, hivyo kuimarika kwa uchumi wa China kumetoa msukumo kwa ukuaji wa uchumi wa kikanda.