Russia yataka uchunguzi ufanywe kuhusu shambulizi dhidi ya Bwawa la Nova Kakhovka
2023-06-09 19:33:36| cri

Baraza la Seneti la Bunge la Russia jana Alhamis limetoa barua ya wito kwa mabunge ya nchi mbalimbali, ikisema kwamba jeshi la Ukraine lililipua Bwawa la Nova Kakhovka, kitendo kinachokiuka sheria ya kimataifa. Russia imetaka uchunguzi kamili ufanywe kuhusu tukio hilo na kudai fidia kutoka kwa pande husika.

Shirika la Habari la Ukraine jana lilisema, nchi hiyo inaamini kuwa jeshi la Russia lililipua bwawa hilo, na tayari imewasilisha mashtaka kwa mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya.