Mkutano wa 10 wa wanaviwanda wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu wafanyika Saudi Arabia
2023-06-12 09:07:03| CRI

Mkutano wa 10 wa wanaviwanda wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu ambao pia ni kongamano la 8 la uwekezaji ulifanyika jana huko Riyadh nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi 3,000 kutoka nchi zaidi 20.

Mkutano huo wa siku 2, ukiwa na kauli mbiu “Kushirikiana kwa China na nchi za Kiarabu na kutimiza ustawi wa pamoja” utajadili masuala ya biashara, fedha, miundombinu, nishati na uhifadhi wa mazingira kwenye mchakato wa uzalishaji viwandani ili kuwezesha kufikiwa kwa makubaliano na kuimarisha ushirikiano halisi.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Bw. Faisal bin Farhan Al Saud, katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Ahmed Aboul Gheit na waziri wa uwekezaji wa Saudi Arabia Bw. Khalid AbudlazizD.Al-Failih walihudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo.

Bw. Faisal alisema kuwa, mkutano huo ni jukwaa muhimu la kuzidisha urafiki wa jadi kati ya nchi za Kiarabu na China na utahimiza ushirikiano wa pande hizo mbili na kujenga mustakabali wa pamoja wa kuwanufaisha watu wa pande hizo mbli na kulinda amani na maendeleo ya dunia.