China yachangia tani zaidi ya 3,500 za nafaka kwa Syria iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi
2023-06-12 08:53:42| CRI

China imetoa tani zaidi ya 3,500 za nafaka kwa Syria, ili kuisadia nchi hiyo iliyoathiriwa vibaya na vita kufufuka kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Februari 6.

Mwenyekiti wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Syria SARC Khaled Hboubati na balozi wa China nchini Syria Shi Hongwei wamehudhuria hafla ya kukabidhi shehena tano za tani 2,336 za ngano na tani 1,180 za mchele iliyofanyika katika makao makuu ya SARC huko Damascus.

Katika hafla hiyo, Hboubati ameishukuru China kwa niaba ya watu wa Syria na SARC kwa kutoa msaada katika mgogoro wa kibinadamu wa nchi hiyo, hasa baada ya tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkubwa katika sehemu ya kaskazini na magharibi ya nchi hiyo na maelfu ya watu kukosa makazi.

Kwa upande wa balozi wa China, amesema kuwa China itaendelea kuipatia Syria msaada wa kibinadamu na itashiriki kwenye mchakato wa ujenzi upya wa nchi hiyo. Pia ana imani kuwa watu wa Syria wataondokana haraka na athari za tetemeko hilo.