Mkutano wa ngazi ya juu wa biashara kati ya China na Honduras wafanyika Beijing
2023-06-12 08:46:48| CRI

Mkutano wa ngazi ya juu wa biashara kati ya China na Honduras umemalizika Jumapili mjini Beijing, ukiwa ni wa kwanza wa aina yake tangu nchi hizi mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi Machi 26. Ujumbe wa watu zaidi ya 200 kutoka nyanja za siasa na biashara wa pande hizo mbili umehudhuria mkutano huo.

Naibu mwenyekiti wa Baraza la Kuhimiza Biashara ya Kimataifa la China Bw. Zhang Shaogang ametoa wito kwa kampuni za nchi hizi mbili kufanya juhudi kwa pamoja ili kuingiza zaidi bidhaa za Honduras zenye ubora wa juu kwenye soko la China, kuendelea kupanua biashara kati ya pande mbili, kuongeza ajira na kuboresha maisha ya watu wa nchi zote mbili.