Ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Ntorya kwenda Kiwanda cha uchakataji cha Madimba mkoani Mtwara, Tanzania, unatarajia kuanza muda wowote kuanzia sasa.
Hatua hiyo imekuja baada ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini humo (TPDC) kukamilisha malipo ya fidia kwa wakazi 225 ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo. Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC, Jacob Haule amesema hayo jana jumatatu katika zoezi la kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi 19 ambao walikuwa wamesalia.
Katika hatua nyingine, Haule amesema zaidi ya shilingi milioni 430 zimetumika kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi huo.