ILO latoa wito wa kuacha kuwatumikisha watoto
2023-06-13 09:24:27| CRI

Tarehe 12 mwezi Juni ni Siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa Watoto. Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) lilifanya mkutano wa ngazi ya juu huko Geneva, Uswisi siku hiyo hiyo, likitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kutokomeza  utumikishwaji wa watoto.

Katika mkutano huu wenye kaulimbiu“Kufikia haki za kijamii na kutokomeza utumikishwaji wa watoto”, washiriki walisisitiza dharura ya kukomesha ajira kwa watoto na kujadili jinsi watakavyoimarisha haki za kijamii.

Akihutubia kwa njia ya video, Mkurugenzi mkuu wa ILO Bw. Hung Bo amesema idadi ya watoto wanaotumikishwa duniani imefikia milioni 160, ikiwa ni karibu moja ya kumi ya jumla ya idadi ya watoto duniani. Kibaya zaidi ni kwamba nusu ya watoto wanaotumikishwa wanafanya kazi za hatari ambazo ni tishio halisi kwa afya yao ya kimwili na kiakili. Amesisitiza ulazima wa kupinga kwa nguvu zote utumikishwaji wa watoto kupitia kuunga mkono haki pana za kijamii.