Kongamano la Uwekezaji kwenye Sekta ya Huduma Barani Afrika (AHIF) lilianza Jumatatu mjini Nairobi, Kenya, huku washiriki wakitafuta njia za kupata uwekezaji katika sekta ya utalii.
Kongamano hilo la siku tatu linawaleta pamoja zaidi ya wajumbe 500 kutoka zaidi ya nchi 40, wakiwemo maafisa wakuu wa serikali, wawekezaji wa sekta ya huduma, na wataalam wa sekta hiyo ili kuonesha fursa katika sekta ya huduma barani Afrika.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi alisema mkutano huo unakuja katika wakati mwafaka ambapo sekta ya utalii barani Afrika inaimarika kutokana na athari mbaya za janga la UVIKO-19. Ameeleza kuwa Afrika iko wazi kwa wale wenye hamu ya kuwekeza na kutumia fursa nyingi zinazopatikana katika Nyanja zinazostawi za sekta ya utalii.
Kwa upande wake Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Urithi, Peninah Malonza, alisema kuwa nchi yake ina nia ya kuvutia wawekezaji zaidi wa kigeni katika sekta ya huduma.