Mashindano ya 22 ya lugha ya Kichina ambayo hufanyika kila mwaka kote duniani, yameanza rasmi Jumapili nchini Rwanda ambapo wanafunzi kutoka shule mbalimbali wameshindana kugombea ubingwa.
Kwenye shindano hilo, washiriki wameonesha upendo, shauku na dhamira yao ya kujifunza lugha, utamaduni na sanaa za China.
Akifungua shindano hilo, Balozi wa China nchini Rwanda Wang Xuekun amesema shindano hilo ni daraja muhimu la mawasiliano linalounganisha China na Rwanda. Kupitia shindano hilo, idadi kubwa ya wanafunzi wa Rwanda wamepata fursa za kuitembelea China, kujionea nchi hii kwa macho yao, na kuwa na njia tofauti ya maisha.