Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) jana limelaani mashambulizi yaliyofanywa na kundi la waasi dhidi ya watu waliokimbia makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kusema kuwa mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu wasio na hatia na watu wengi kupoteza makazi yao.
Kwa mujibu wa UNHCR, watu wenye silaha jana walishambulia kambi ya wakimbizi mkoani Ituri, na kusababisha watu wasiopungua 45 kuuawa, wakiwemo watoto na wanawake, na kwamba watu wasiopungua 12 wameuawa kwa kuungua baada ya makazi yao kuchomwa moto.