China kuendelea kushirikiana na Kenya katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa jangwa
2023-06-13 21:21:58| cri

Profesa Robert Gituru ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha kilimo na teknolojia cha Jomo Kenyatta nchini Kenya na mkurugenzi mwenza wa kituo cha pamoja cha utafiti baina ya China na Afrika SAJOREC,amesema China itaendelea kushirikiana na Kenya katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa jangwa.

Profesa Gituru anasema ushirikiano huo wa nchi hizo mbili utasaidia katika kuhakikisha ardhi zilizogeuka jangwa zinazalisha vyakula zaidi kwa faida ya mamilioni ya raiya.

Profesa huyo ambaye pia ni mtaalam wa mazingira anasema China imesaidia siyo tu Kenya bali bara la Afrika katika mchakato wa kurejesha ardhi za jangwani na badala yake sasa kuwa maeneo ya kuzalisha chakula na kueneza misitu.