Mamlaka ya taifa ya usimamizi wa ukame nchini Kenya imetoa ripoti ikisema, idadi ya wakenya wanaohitaji msaada wa chakula katika maeneo kame imefikia milioni 4.4, huku maeneo hayo yakikabiliwa na uchelewaji kati ya ufufukaji kutokana na ukame na upatikanaji wa chakula.
Mamlaka hiyo imeeleza kuwa uchelewaji huo umeendelea kuwafanya mamia ya wakazi kuwa na utapiamlo.
Mbali na hayo, mamlaka hiyo imesema kuwa mvua katika maeneo mengi kame ilisababisha mafuriko makubwa na kuleta athari mbaya kwa maisha ya wakazi wa huko.
Imeongeza kuwa hali ya chakula huenda haitaboreka katika maeneo hayo, kwa kuwa uchunguzi wa hali ya mvua unaonesha kuwa sehemu kadhaa za maeneo kame zimepata kiasi kidogo cha mvua cha milimita 75 hadi 11 kikilinganishwa na kiwango cha kawaida.